Ni filamu yenye kisa cha aina yake ikiwa imewakutanisha nyota kadhaa akiwamo Riyama Ally,Yusuph Mlela (Johnson),Slim Omary na Faudhia Abdala(Chausiku) ambaye amecheza kama mhusika mkuu.
Kisa kikuu kwenye filamu hii kimebebwa na Chausiku ambaye amecheza kama msichana wa uswahilini, anaendeesha maisha yake kutokana na biashara ya ukahaba.
Chausiku ana majirani wengi mtaani kwake kutokana na tabia ya kuchukua wanaume za watu na kupenda ugomvi.
Pamoja na tabia yake hiyo anaonekana pia kuwa mbinafsi, kwani haonyeshi kumjali mdogo wake Adrian anayekabiliwa na matitizo kadhaa ikiwamo kuumwa na kufukuzwa shule kutokana na kukosa ada.
Wanawake wa mtaa huo wanamfanyia kila aina ya hira kumkomesha, lakini Chausiku anaonekana kukubuhu na kuwamaliza wanaume wote wa wapangaji wenzake.
Johson ndiye anayeonekana kujali hali ya Adrian licha ya kuwa naye anamsaidia kwa kuwa anampenda Chausiku, lakini mwanamke huyo hamtaki kutokana na kipato chake kidogo anchokipata kutokana na kazi ya kushona viatu.
Chausiku hataki hata kwenda hospitali kumjulia hali mdogo wake, hivyo inamlazimu Johnson kumuuguza mpaka anapopona na kumhamishia nyumbani kwake.
Dada mtu anafukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi, lakini hamalizi muda mrefu anapata mwanaume mwingine anayemtafutia nyumba nyingine.
Kama kawaida yake huko nako anaendeleza tabia yake anawamaliza wanaume wote wa nyumba hiyo.
Halima rafiki wa karibu wa Chausiku ndiye anayeikomesha tabia hiyo na kufikia uamuzi wa kumroga kwa kumtia upofu baada ya kubaini kuwa anamuibia mwanaume wake.
Ni filamu ambayo imetawaliwa na mambo mengi huku sehemu kubwa ikilenga kuonyesha maisha ya uswahilini.Kwa uhondo zaidi itafute ujionee kilichomo ndani yake.
Imeandaliwa na Elizabeth Edward
No comments:
Post a Comment