Monday, 26 January 2015

Maajabu ya damu ya Yesu

MAAJABU YA DAMU YA KUNYUNYIZA YA YESU; OMBA KWA KUTUMIA DAMU YA YESU UTASHANGAA KUPATA MATOKEO YAFUATAYO!
Wakati Waisraeli Wakiwa Utumwani, Mungu Alipiga Pigo La Kumi Na La Mwisho, Lakini Pigo Lilifanyika Kwa Imani Kupitia Damu Ya Kondoo Ambaye Walimpa Jina La Pasaka; Ambaye Kwa Agano Jipya “YESU KRISTO NI PASAKA WETU AMBAYE AMEKWISHACHINJWA”
Walipotumia Damu Ya Yesu Kwa Kupaka MIMO YA MAMALANGO KWA IMANI, Yalitokea Mambo Kadhaa:
1.Wote Waliokuwa Ndani Ya Nyumba Za Waisraeli Zilizopakwa Kwa Damu Ya Pasaka [Damu Ya Yesu Kwa Agano Jipya] HAWAKUPATWA NA MAUTI YA WAZALIWA WA KWANZA WAO.
Ripoti Ya Vifo Vya Wazaliwa Wa Kwanza Wa Misri Haikuwagusa Waisraeli; MHARIBU [SHETANI KWA AGANO JIPYA] Alipopita KUsababisha Vifo Na Mauti, HAKUWEZA KUINGIA KWENYE NYUMBA ZA WAISRAELI!

Friday, 23 January 2015

Kanuni ya Kumjua Mungu

Kanuni ya kumjua Mungu ipo hivi:

Hauwezi kuja kwa Yesu bila kuitwa na YEHOVA ~ (YOHANA 6:44;65); hauwezi kumjua Roho Mtakatifu bila kufundishwa na Yesu ~ (YOHANA 15:26); hauwezi kumpokea Roho Mtakatifu bila kupewa na Yesu ~ (YOHANA 20:22); na hauwezi kwenda kwa YEHOVA bila kuongozwa na Yesu ~ (YOHANA 14:6).

Zingatia kwamba; Pasipo Yesu hauwezi kufanya lolote ~ (YOHANA 15:5); na pia kila mtu asiye na Roho Mtakatifu ndani yake huyo si mwanafunzi wa Yesu. ~ (WARUMI 8:9).

Ni lazima kwanza KUITWA NA YEHOVA, pili KUMPOKEA YESU, na ndipo utakapompata Roho Mtakatifu; Naye Roho Mtakatifu akaapo ndani yako daima ndipo unapata uzima wa milele. 

Inawezekana ukawa jambo hili usilielewa hata ukajiuliza;

Thursday, 22 January 2015

DHAMBI

DHAMBI ISIYO SAMEHEWA...! ! !
Bwana Yesu amesema kwamba: "...Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa." - (Mathayo 12:31)
Je! Nini maana ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?
 Tukianza na neno KUFURU, maana yake ni: Kusema maneno yakumtukana Mungu au kufanya matendo yanayomtukana Mungu. Tukiendelea kusoma Mathayo 12:32tunaona Bwana Yesu anasema kwamba:
"Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao." (Mathayo 12:32)
Ni kweli kuwa Yesu ni Mungu; lakini, Je! Yesu anamaanisha nini kuhusu dhambi isiyosamehewa ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?

MSAMAHA

SOMO: - MSAMAHA
Tukisoma kitabu cha WAEFESO 4:31,32 tunaona Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, MKASAMEHEANE kama na Mungu katika Kristo ALIVYOWASAMEHE ninyi." (Efe 4:31,32)
Je! Nini maana ya neno MSAMAHA na kuna faida zipi katika KUSAMEHE; na kwa nini tunapaswa KUSAMEHE?
MSAMAHA:
Neno “MSAMAHA” ni neno jepesi kulitamka lakini ni pana sana katika maana. Nisemapo "NI NENO JEPESI KULITAMKA" ninamaanisha kulitamka tu kwa kawaida na katika hali ya kawaida tu pasipo kukosewa, lakini kwa watu wengi; neno MSAMAHA ni neno gumu sana kulitamka toka rohoni mwao hususani pindi wanapokosewa. Nilifanya utafiti juu ya hili neno nikagundua zipo siri kubwa sana katika KUSAMEHE ambazo Shetani apendi watu wazifahamu.

Meneja Misamaha ya Kodi TRA

Dar es Salaam.  Meneja Misamaha ya Kodi TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa anayekabiliwa na kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh 1.6 bilioni kutoka akaunti ya Tegeta Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Hakimu Mkazi, Frank Moshi jana alimuachia huru Mutabingwa baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwasilisha fedha taslimu Sh 1bilioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Mutabingwa aliachiwa huru kwa dhamana baada ya kuwasilisha  hati tano za nyumba za watu tofauti tofauti  zenye thamani ya Sh 1.332 bilioni, wadhamini watatu ambao kati yao wawili walikuwa wafanyakazi wa TRA na mmoja mjasiliamari.

Kura ya maoni

Kwa nini ni vigumu kura ya maoni kufanyika Aprili
*Jaji Warioba aonya mchakato kwenda kinyume na Sheria akibainisha athari zake kuwa ni vurugu katika uchaguzi mkuu.
Wakati Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ukisubiri hatua ya kura ya maoni, wengi wameendelea kutoa maoni yao yanayoonyesha kutofautiana kimtazamo.
Lakini hiyo ndiyo demokrasia ambayo mwisho wa siku hukumu ya kupita au kutopita kwa Katiba Inayopendekezwa itatolewa Aprili 30 mwaka huu kwa kura ya NDIYO na HAPANA.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ni miongoni mwa watu wanaoendelea kutoa maoni yao kuhusu suala hilo. Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa makala haya, Jaji Warioba anaonya kuwa maandalizi hayaonyeshi uwezekano wa kura ya maoni kufanyika kwa tarehe iliyopangwa.

Wednesday, 21 January 2015

Panya Road

Panya Road katika jicho la Tehama

Ilikuwa jioni muda wa saa tisa hadi kumi baadhi ya watu walioko katikati ya jiji la dar es salaam walipokea ujumbe mfupi kwenye simu zao kwamba kundi la Panya Road limeteka baadhi ya mitaa na wanatishia watu.
Nao waliopata ujumbe kwa njia ya simu walianza kuweka kwenye mitandao ya mawasiliano hasa ya kijamii. Kwahiyo watu wengi walianza kutoka katikakati ya jiji la Dar es Salaam kwa kasi kwa sababu ya woga waliokuwa nao dhidi ya kundi hili.
 Katika baadhi ya maeneo kama Ubungo na Sinza, maduka yalifungwa na biashara nyingine zilisimama kwa kuhofia vijana hawa.

Tehama Tanzania

Maendeleo ya kuridhisha ya Tehama Tanzania
Pamoja na kuwa nchi ya tatu katika ukanda wa Afrika Mashariki katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (Tehama), jitihada za uwekezaji na matumizi katika teknolojia hiyo, yanatajwa kuipandisha chati Tanzania kimataifa.
Nuzulack Dausen, Mwananchi
Huenda usijue nini kinaendelea wakati unatumia mtandao ofisini kwako au nyumbani kupitia kompyuta, tabiti au simu ya mkononi.

Mbegu za Limao

Umuhimu wa mbegu za limao


Unafahamu kuwa mbegu za limao zina faida lukuki kiafya? Wakati mwingine unaweza ukawa unatupa kitu bila kujua kuwa kinaweza kuwa na umuhimu gani kiafya.

Mfano mzuri wa vitu hivyo ni mbegu za limao,ni wachache ambao wanatumia limao na kuhifadhi mbegu hizi.

Hilo linatokana na wengi kutojua umuhimu wa mbegu hizi katika mwili na kujenga  afya ya binadamu .