Afya

 SMOOTHIES YA STRAWBERRY  NA NDIZI


Assalam Aleykum ndugu zangu naimani wote mko salama  kwa uwezo wake mungu na mlio kuwa wagonjwa mungu atawasaidia mtapona kwa Baraka zake.
Leo ningependa kuwaletea kitu kingine naimani kwa wengi huwa ni kitu kigeni japo kuwa kuna wakati nilitoa kitu kama hiki na nilipata simu nyingi sana kwa watu kuniuliza kinywaji hicho, maana kilikuwa ni kigeni kwa asilimia kubwa.
 Smoothies ni mchanganyiko wa matunda na maziwa na hufanya kinywaji hiki kuwa kizito ni nzuri sana kwa watu wa kila rika isipokuwa mtoto mchanga  jaribu na uone mafanikio yake.

MAHITAJI
Pakti moja ya maziwa mtindi ya nusu lita
Strawberry  kikombe kimoja
Ndizi mbivu mbili
Maziwa ya unga nusu kikombe
Maji baridi nusu kikombe
 Asali vijiko vine hadi vitano 
Cubes nne
Vanilla ya maji matone matatu hadi manne (chunga usijaze na usiweke vanilla ya unga)
                 JINSI YA KUTENGENEZA
Chukua jagi la blender weka vitu vyote ispokuwa bakisha strawberry kama mbili hadi tatu za kupambia kisha saga mpaka isagike na kuona iko tayari kabisa kisha weka kwenye maglass na  itakuwa tayari kunywewa, ni nzuri kwa afya yako fanya utaona mabadiliko kiafya mpaka ngozi yako.
             Imeandaliwa na Mtaalam wa Mapishi
            Filsan Ally Mohamed
           Mawasiliano 0652055925
           mapishiyafilsan@gmail.com

No comments:

Post a Comment