Music

Zari na Diamond mguu kwa mguu
 
KATIKA mambo ambayo yanawaacha hoi wapenzi wa pea ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu, ni ukaribu uliopo hivi sasa kati ya Zarina Hassan maarufu Zari ‘thebosslady’ na nyota huyo wa muziki Afrika kwa sasa.
Zari ambaye alianza kuonekana na mkali huyo tangu katika utolewaji wa tuzo za Channel O mwezi Novemba, amekuwa akimsindikiza Diamond katika kila shoo anayokwenda hivi sasa, ukilinganisha na ilivyokuwa kwa mpenzi wake wa siku nyingi Wema Sepetu.

Wiki hii Zari ameonekana na Diamond katika ziara yake ya nchi za Burundi na Rwanda ambako walitembelea makumbusho mbalimbali yakiwamo ya Kimbari.
Staa huyo kutoka Kampala Uganda, alibubujikwa na machozi baada ya kutembelea makumbusho hayo nchini Rwanda.
Zari alikuwa ameongozana na mpenzi wake huyo, ambaye alikuwa akifanya ziara katika nchi za Burundi alikofanya shoo Bujumbura Desemba 30 na Rwanda ambako alifanya shoo Januari 1.

No comments:

Post a Comment