Umuhimu wa mbegu za limao
Unafahamu kuwa mbegu za limao zina faida lukuki kiafya? Wakati mwingine unaweza ukawa unatupa kitu bila kujua kuwa kinaweza kuwa na umuhimu gani kiafya.
Mfano mzuri wa vitu hivyo ni mbegu za limao,ni wachache ambao wanatumia limao na kuhifadhi mbegu hizi.
Kwa mujibu wa jarida la Live and Feel mbegu za limao zinaweza kutumika kama kinga na tiba ya aina mbalimbali za fangasi.
Mbegu za limao zimekuwa zikitumika kama kirutubisho kwenye losheni na mafuta mbalimbali ya kupaka mwilini.
Virutubisho vya vitamin C vilivyomo ndani ya mbegu za limao husaidia kung’arisha ngozi na kuifanya iwe yenye afya.
Unawezaje kula mbegu za limao
Wote tunafahamu kuwa mbegu hizi zina uchungu hivyo inashauriwa unapokula uchanganye na kitu kingine.
Mfano unaweza kuzisaga mbegu hizi na kuzichanganya na kuzichemsha pamoja na maziwa.
Imeandaliwa na Elizabeth Edward

No comments:
Post a Comment